26 Nov, 2026
PPRA AND THE OFFICE OF THE ATTORNEY GENERAL TO STRENGTHEN LEGAL COMPLIANCE IN PUBLIC PROCUREMENT
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) yenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kisheria yanayohusiana na michakato ya Ununuzi wa Umma kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki (NeST) na LSMIS.
Hafla ya utiaji saini imefanyika leo, Novemba 26, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya jitihada za taasisi hizo kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Bw. Dennis Simba, amesema kusainiwa kwa hati hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha ufanisi wa sekta ya Ununuzi wa Umma na kuhakikisha kuwa michakato ya ununuzi inatekelezwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria.
Bw. Simba ameeleza kuwa matumizi ya mifumo hiyo katika usimamizi wa mikataba ni miongoni mwa hatua muhimu za kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika Ununuzi wa Umma, kwani husaidia kurahisisha michakato ya kazi, kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza katika hatua mbalimbali.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari ameipongeza PPRA kwa jitihada inazoendelea kuchukua katika kuimarisha uzingatiaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma na kuboresha mifumo ya usimamizi wa shughuli za ununuzi nchini.