Sunday, August 07, 2022
   
Text Size

Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dkt. Irene Isaka, ametoa wito kwa wataalam wa ununuzi na ugavi, kutoa maoni kwa Mamlaka juu ya namna ya kuongeza ukidhi wa sheria ya ununuzi wa umma. (PPRA).

Dkt. Isaka alitoa wito huo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (APSP), uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2021 jijini Arusha. Aidha, Dkt. Isaka alisisitiza juu ya umuhimu wa ushirikiano endelevu utakaowawezesha wanataaluma hao kutekeleza majukumu yao kwa weledi na hivyo kufanikisha juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa ufanisi.

“Mamlaka itafurahi sana endapo itapata maoni yenu juu ya namna bora ya utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma ili tuweze kuwasaidia kuongeza kiwango cha ‘çompliance’ ya sheria hii,” alisema Dr. Isaka na kuwaomba ushirikiano ili kwa pamoja wafanikishe utekelezaji mzuri wa mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano.

Afisa Mtendaji Mkuu alisema pia kwamba ushirikiano wa wataalamu hao ni muhimu sana katika kufanikisha malengo ya Serikali katika miradi ya kimkakati, “ambayo tungependa utekelezaji wake ufanyike kwa ufanisi na kwa wakati, lakini pia kwa kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma.”

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, aliwataka wanataaluma hao kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weledi huku wakiweka sawa uwiano kati ya mahitaji ya biashara na miongozo ya sheria na kanuni za ununuzi wa umma, ili kuendana na kasi ya mabadiliko na mahitaji kwenye maeneo yao ya kazi.”

“Taaluma hii lazima iendane na uelewa wa biashara ili muwe kwenye wakati mzuri wa kushauri, fanyeni kazi kwa weledi mkubwa na kemeeni vitendo vya rushwa,” alisema Bi. Zaipuna.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, Bw. Emmanuel Urembo, amesema chama hicho kimeunda kamati nne zitakazohusika na mafunzo, uzingatiaji wa sheria ya ununuzi wa umma, usimamiaji maadili, na ushauri. “Pamoja na mambo mengine tumeunda kamati itakayosimamia mambo ya uzingatiaji wa sheria ya ununuzi na kanuni zake, na itatoa ushauri wa kitaalamu pale itakapobainika kuna jambo la kubishaniwa,” alisema Bw. Urembo.

Katika mkutano huo, chama hicho, chenye jumla ya wanachama 295, kilizindua huduma ya bima ya mkono wa pole itakayosaidia mwanachama pale atakapopatwa na msiba wa ndugu yake, ambapo APSP imewadhamini wanachama wake wote.

En cilgin hd porno videolari icin sitemizi ziyaret ediniz.Yerli yabanci escort bodrum kizlari burada