Monday, May 16, 2022
   
Text Size

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuwaandikia barua wakuu wa taasisi za umma ambazo hazijaunganishwa ili kutumia mfumo wa ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao (TANePS) kueleza sababu za wao kukaidi matakwa hayo ya kisheria pamoja na maagizo ya Serikali.

Waziri Nchemba ametoa agizo hilo tarehe 29 Septemba jijini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya tathmini ya utendakazi wa PPRA kwa mwaka wa fedha 2020/21, ambapo amesema Serikali imeweka mkazo katika uchumi wa kidigitali, ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwenye mifumo ya kielektroniki, na kwamba haitavumilia watu wanaokwamisha malengo hayo. “Natoa agizo kwa wakuu wa taasisi ambazo hazijaunganishwa kwenye mfumo [TANePS] na ambazo haziutumii kwenye michakato ya ununuzi, kuleta kwangu sababu za kukaidi maagizo hayo ya Serikali ambayo pia yanatokana na sheria ya ununuzi wa umma,” alisema Dkt. Nchemba.

Waziri aliendelea kwa kusema ni bora wanaoona ugumu katika kutumia mifumo ya kielektroniki wawapishe wale wanaoweza kuliko kukwamisha matumizi yake. Waziri huyo alimuagiza pia Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, kuzuia, kama inawezekana, malipo ya ununuzi wowote uliofanyika nje ya TANePS. “Kwa kushirikiana na PPRA, mzuie malipo ya manunuzi yanayofanywa nje ya TANePS, isipokuwa kama yana kibali maalum cha wizara,” aliongeza Dkt Nchemba.

Akizungumza awali kabla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa niaba ya Mwenyekti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Prof. Ninatubu Lema, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo, alibainisha kuwa pamoja na ukweli kwamba taasisi nyingi zimeshaunganishwa na mfumo TANePS, ni chache sana ambazo zinautumia kuchakata ununuzi.

“Taasisi 130 kati ya 718 zilizokuwa zimeunganishwa, hazikuwasilisha mipangomwaka ya ununuzi kupitia mfumo huu. Aidha, taasisi 208 ziliwasilisha mipangomwaka ya ununuzi kupitia TANePS lakini hazikuchakata zabuni kupitia mfumo huu,” alisema Prof. Lema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, alisema kuna umuhimu wa kuziwajibisha taasisi ambazo hazitumii TANePS, pamoja na kuzijengea uwezo.

“Itabidi tuangalie namna ya kuwawajibisha wahusika, na kama sababu ni uwezo mdogo basi tuone namna ya kuwajengea uwezo,” alisema Bw. Tutuba

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wastani wa ukidhi wa sheria ya ununuzi wa umma kwa taasisi 85 zilizokaguliwa umeshuka kwa asilimia 3.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambao ulikuwa asilimia 78.8. Taasisi kumi zilizofanya vizuri ni pamoja na Mfuko wa Hifadhi kwa Watumishi wa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Makao Makuu, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Wizara ya Fedha na Mipango, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Ofisi ya Katibu Tawala Arusha, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Taasisi zilizofanya vibaya ni Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Halmashauri za Wilaya za Mbogwe, Biharamulo na Chato, pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama (Tanzania Livestock Research Institute).

Pia, ukaguzi maalum uliofanywa katika kipindi husika umeonesha kuwa Serikali itaokoa kiasi cha shilingi bilioni 1.17 endapo mapendekezo yaliyotolewa yatazingatiwa na kutekelezwa ipasavyo. Aidha, Serikali ilipata hasara ya shilingi milioni 580.27 iliyotokana na kutunza viuatilifu baada ya muda wa matumizi, kutokutoza fidia zinazotokana na ucheleweshwaji wa huduma, bidhaa au kazi, gharama zisizo za lazima kwa kuchapisha matangazo, na gharama za ziada baada ya kurejewa kwa mchakato wa zabuni bila sababumsingi.

En cilgin hd porno videolari icin sitemizi ziyaret ediniz.Yerli yabanci escort bodrum kizlari burada