Wednesday, September 28, 2022
   
Text Size

Ilikuwa ni majira ya jioni ya tarehe 17 Julai, 2021 pale Mhandisi Mary Swai, aliyekuwa akikaimu nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, alipotumia kundi sogozi la ‘WhatsApp’ kuwafahamisha Wafanyakazi wa Mamlaka kuwa Afisa Mtendaji Mkuu - Mhandisi Leonard Saasita Kapongo amefariki dunia katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Muda mchache baadaye, taarifa hizo zilisambaa kwa wadau mbalimbali hususani wa ununuzi wa umma, wengi wakiwa hawaamini, lakini siku zote Kazi ya Mungu haina makosa.

Ni tarehe 28 Oktoba, 2018, Mhandisi Leonard Saasita Kapongo alipoteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Awamu ya Tano, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Wafanyakazi wa PPRA tunaikumbuka sana siku aliporipoti Ofisi za Makao Makuu ya PPRA jijini Dodoma na kukutana nasi kwa mara ya kwanza kwenye kikao cha watumishi tarehe 12 Novemba, 2018. Tunakumbuka alipotumia kikao hicho kuwatoa hofu watumishi juu ya changamoto zinazowakabili wao na Taasisi kwa ujumla na kwamba suala la ustawi wa Taasisi na Watumishi wake litakuwa ni miongoni mwa vipaumbele vyake. Hakika, kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejementi, alisimamia vilivyo suala la maslahi ya watumishi, na ameondoka akiwa hana deni kwao.

Utendaji wake ulilenga pia kuimarisha ushirikiano na Taasisi nyingine za umma zikiwemo Wizara Mama ya Fedha na Mipango, Taasisi zinazohusika moja kwa moja kwenye usimamizi wa sekta ya Ununuzi wa Umma kama vile PPAA, PSPTB na GPSA. Jukumu ambalo alilitendea haki.

Chini ya uongozi wake pia, mashirikiano kati ya PPRA na Bunge yaliimarika kutokana na namna alivyofanya kazi karibu na Kamati zake za Bajeti na ile ya Hesabu za Serikali.

Wadau wa Ununuzi wa Umma kutoka ndani na nje ya Nchi watamkumbuka daima kwa namna alivyoshirikiana nao katika kazi na matukio mbalimbali yaliyokuwa na lengo la kuboresha sekta ya ununuzi wa umma, ikiwemo Kongamano la Mwaka la Usimamizi kwenye Sekta ya Ununuzi wa Umma, Jukwaa la Ununuzi wa Umma kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu. Alitoa kipaumbele kwenye matukio hayo kwa kuwa aliamini yanatoa fursa kwa wadau kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya ununuzi wa umma na hatimaye kuzipatia ufumbuzi.

Tutaendelea kumkumbuka kwa namna alivyotekeleza majukumu yake kwa weledi, unyenyekevu, ucheshi na usikivu wa hali ya juu kwa walio juu yako na chini yako.

PPRA itaendelea kuhakikisha kuwa Ununuzi wa Umma unakuwa na tija kwa ustawi wa Watanzania na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

ENDELEA KUPUMZIKA KWA AMANI MHANDISI LEONARD SAASITA KAPONGO

En cilgin hd porno videolari icin sitemizi ziyaret ediniz.Yerli yabanci escort bodrum kizlari burada